MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUWA NAYO WAKATI WA KU-APPLY CHUO NA GHARAMA ZAKE

Uhali gani mpenzi msomaji wa blog yangu,natumai umzima wa afya tele karibu katika muendelezo wa taarifa muhimu zinazoendelea kutolewa na blog yangu.
Kwanza kabisa ,napenda kuwapongeza wote mliofanikiwa kutimiza vigezo vinavyo hitajika kudahiliwa na vyuo mbali mbali nchini,kwaajiri ya kujiunga na elimu ya vyuo vikuu nchini,kwa mwaka mpya wa masomo 2017/2018.

  Leo blog yako ya Lufametz ,katika muendelezo wake wa kukupa taarifa muhimu ,tunakuletea taarifa muhimu Kwa mtu yeyote anayetaka ku-apply chuo chochote nchini.

A. MAHITAJI MUHIMU WAKATI WA KU-APPLY
      1).Passport size
           Katika kila chuo utakacho omba utatakiwa kuambatanisha na picha yako passport size  (1),muombaji au mtu anayekusaidia kufanya maombi atatakiwa kui-scan picha hiyo na kuiambatanisha kwenye form yako ya maombi.
      2).Namba zako za mtihani wa kidato cha nne na cha sita
        NB: Kwa wale watakao omba degree Kwa kutumia  cheti cha diploma watatakiwa kuomba kwanza NACTE (gharama ni 20,000/=) ili apewe code number yake ,ambayo ndiyo atakayo itumia kuomba degree.
   Pia kwa wale walio rudia mtihani watatakiwa kuandika namba zao za mitihani yote ya kwanza na ile aliyorudia.
     3).Taarifa zako binafsi
          -Tarehe yako ya kuzaliwa
          -mwezi na mwaka
       4). Email na namba yako ya Simu
              Hii pia huitajika wakati wa kuomba. Kwani hutumika baadae kwaajiri ya kukupa taarifa muhimu za chuo.
        5) Pesa
               Unashauriwa kuandaa pesa kuanzia Tsh 150,000/= Kwa wale watakao taka kuomba kwenye vyuo votano . Pesa hizo ni lazima ziwe kwenye account itakayo tumika kulipia form hiyo. Kwa mantiki hiyo unashauriwa pesa hizo ziwe kwenye account ya Tigo pesa, M.pesa airtel money n.k

B.GHARAMA ZA FORM HIZO ZA KUOMBA NAFASI ZA CHUO
      Baada ya kwa mabadiliko haya yaliyoko sasa .kila muombaji atatakiwa kuomba kwenye chuo husika moja Kwa moja ,na malipo yatafanyika kwenye chuo hicho kulingana na bei walizojiwekea .

 Ila mpaka sasa 90% ya vyuo vyote nchini, vinatoa form hizo Kwa Tsh 30,000/= mfano .UDOM 30,000/=
             MZUMBE  30,000/=
             UNIVERSITY OF IRINGA 30,000/=  N.K

C.IDADI YA FACULTY (KOZI ) UNAZO RUHUSIWA KUOMBA KWENYE CHUO KIMOJA
        90% Ya vyuo vyote nchini vinatoa nafasi tano. Kwahiyo muombaji ataweza kuomba faculty tano tofauti kwenye chuo kimoja.

D.MUDA ULIYOTOLEWA  KU-APPLY
         kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyo tangazwa na TUC .vyuo vitaendelea kupokea maombi kuanzia tar 22/07/2017 mpaka tar 30/08/2018 .ikiwa ni zaidi ya mwezi mmoja.


USHAURI
 Kabla ya ku-apply chuo chochote nchini. Hakikisha umepitia vizuri kitabu cha maelekezo kilichotolewa na TUC (TCU guide book) ukizingatia mambo muhimu yafuatayo;
  a).Je kwenye faculty unayotaka kuomba umetimiza vigezo vinavyo hitajika kwa ufasaha?
  b).Je faculty unayotaka kuomba inatolewa kwenye chuo hicho?
  c).Je unataarifa muhimu juu ya faculty unayoitaka?

Kama moja kati ya hayo bado hauko vizuri ni bora utulie kwanza ufanye uhakiki wa taarifa zako kabla hujajaza kuomba nafasi. Kwani unaweza kupoteza pesa bila mafanikio yoyote. Usikurupuke kuchukua maamuzi haraka bila kujiridhisha kwani hapo unachagua maisha yako ya baadae. Muda bado upo wa kutosha ni zaidi ya mwezi tulia ufanye chaguzi sahihi sehemu sahihi.

Ahsante sana Kwa kutembelea blog yangu. Natumai umefanikiwa na kufaidika kupitia chapisho hili .karibu tena Kwa taarifa muhimu zinazotolewa na blog yangu hii.

Huruhusiwi kukopi wala kupest taarifa yoyote kwenye blog hii, bila idhini ya mmiliki wa blog hii **Peter Lugendo ***
www.lufametz@gmail.com
www.Facebook.com/lufametz
www.YouTube.com/lufame TV