- JE, UTAOMBA MKOPO WA ELIMU YA JUU MWAKA HUU?
- • ZIFUATAZO NI SIFA KUMI (10) ZA MSINGI
- 1. Mwombaji awe Mtanzania.
- 2. Mwombaji awe ameomba kudahiliwa na Chuo Kikuu au Taasisi ya Elimu
- ya Juu inayotambuliwa na Serikali.
- 3. Asiwe mwanafunzi wa masomo ya jioni (Part time Student).
- 4. Asiwe na udhamini/ufadhili/msaada wa kifedha kutoka katika vyanzo
- vingine.
- 5. Awe ameomba mkopo kupitia mfumo wa mtandao (OLAMS).
- 6. Awe amefaulu mitihani ya mwisho wa mwaka (wanaoendelea na masomo)
- na matokeo yake kuwasilishwa Bodi ya Mikopo na chuo chake.
- 7. Awe amemaliza Kidato cha Sita au awe na sifa linganishi (kama Diploma
- n.k) ndani ya miaka mitatu (2015/2016 – 2017/2018).
- 8. Awe na umri usiozidi miaka 30 wakati wa kufanya maombi.
- 9. Waombaji ambao wazazi wao ni Wakurugenzi au Mameneja Waandamizi
- katika Makampuni binafsi yanayotambuliwa na Mamlaka za Mapato na
- Usajili hawatarajiwi kuomba;
- 10.Waombaji ambao wazazi wao ni viongozi wa umma au kisiasa ambao
- wanatajwa na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma hawatarajiwi
- kuomba mikopo.
- Mwisho wa kuomba mkopo in Septemba 4, 2017
- Imetolewa na
- Bodi ya mikopo Kwa wanafunzi wa elimu ya juu
- Tanzania HESLB
- Na kuandikwa na Peter lugendo
BREAKING NEWS
Subscribe to:
Posts (Atom)
No comments:
Post a Comment