Uhali gani ndugu msomaji wa makala hii, ni matumaini yangu uumzima Wa
afya tele. Karibu kwenye somo la leo ,kuhusu namna unavyo weza
kuzitumia FURSA zisizo hitaji mtaji mkubwa kujikwamua kimaisha..
Katika
hali ya kawaida kila mwanadamu anacho kitu anachoweza kukifanya Kwa
ufanisi mzuri zaidi lakini hushindwa kuyafanya kutokana na sababu mbali
mbali,kama vile kutojiamini, kushindwa kujitambua vizuri, hofu ya
kushindwa, au kukosa MTAJI ili kufanikisha jambo hilo . Katika mambo
yote hayo tatizo LA kukosa mtaji ndiyo tatizo linalo wasumbua watu
wengi. Kwa kulijua hilo blog yako ya lufametz ,wameamua kukuonesha fursa
12 ambazo unaweza kujihusisha nazo Kwa kutumia mtaji mdogo sana na
kujikwamua kimaisha...**
(1).KUUZA NGUO ZA MITUMBA
fursa
hii haina ulazima wa kuanza Kwa mtaji mkubwa sana ,kwani unaweza kuanza
na mtaji wa hata Tsh 15000/= Mfano yapo masoko kama vile
tandare,karume ,mbagala na masoko mengine mikoani ambayo huuza nguo kwa
bei ya chini sana ,kuanzia tsh 500/= mpaka tsh 1000/= ambazo wewe
unaweza kuzinunua na kuzipeleka sehemu nyingine ambako utaweza kuziuza
kuanzia 1500/= mpaka 2000/= nakukufanya ujikwamue kidogo kidogo huku
ukiplan jambo kubwa zaidi..
(2).KUUZA MAYAI
[image_1]
si lazima uuze wewe kama unahisi huwezi,na unaweza kuanza Kwa mtaji
mdogo tu wa tray hata mbili(2) ukampa mtu akuuzie Kwa bei ya @500/=
..utaweza kuingiza tsh 12000/= Kwa tray moja, ukamlipa 2500/=
aliyekuuzia ikabaki tsh 9500/= na jumla ya faida ikawa tsh 4500 mpk 4000
Kwa kila tray...Kwa namna hiyo utaweza kuongeza tray la tatu nakubakiwa
na tsh 3000/= mkonon huku mtaji ukizidi kukua,hata kukuwezesha kufanya
jambo jingine.
(3).KUUZA MIHOGO,VIAZI,MAHINDI N.K
Hasa
yakukaanga na mahindi huweza kuwa yakuchoma au kuchemsha. Tatizo la
vijana wengi hujiangalia zaidi katika hali ya ubishoo na usister duu
,hivyo kujikuta wanachagua fursa za kuanza nazo mwisho wake wanalalama
kuwa hakuna fursa ..Biashara hii huweza kuanza Kwa mtaji mdogo tu wa tsh
10000/= au 15000/= nakukulipa vizuri kwani hizo ni bidhaa chakula
ambazo ni lazima zitumike kila siku...
(4).KUUZA VINYWAJI VYA JUMLA
Unaweza
ukahofia kuwa utahitaji kuwa na mtaji mkubwa sana ,ila hapana ,unaweza
kuanza Kwa katon au kreti tano tu za soda ,na zitakapoisha utaweza
kuongeza katon moja ...Na Kwa namna hiyo msingi wako utazidi kukua siku
hadi siku nakufikia malengo...
(5).KUFUNDISHA TUISHENI
kama
wewe ni kijana mwenye elimu inayotosha kufundisha wengine ,unaweza
kujishughulisha na kufundisha Kwa kuwatoza pesa unao wafundisha na ikawa
ni fursa pia kukufikisha kwenye malengo makubwa zaidi..
(6).KUANZISHA KIKUNDI AU KAMPUNI YA UZOAJI TAKA.
fursa
hii inalipa kwasababu .kwanza haina watu wengi wanayojihusisha nayo.
Pili taka ni vitu vinavyokuwepo Kwa wingi sana hasa kutokana na shughuli
mbali mbali za kibinaadam .sio lazima ufanye wewe unaweza kuwa kama
organiser au mmiliki wa kampuni hiyo na ukafanikiwa.
(7).KUUZA MAGAZETI
Fursa
hii huenda ikawa rahisi zaidi kwani unaweza kuanza hata Kwa kukopeshwa
magazeti.kisha ukawa unalipa baada ya kumaliza au jioni kufika.unaweza
kuuza Kwa kutembeza au kuweka sehemu moja,na bado ikakulipa hata
kukuwezesha kufikia malengo yako.
(8).KUFUNGUA SEHEMU YA KUFANYISHA WATU MAZOEZI
Sio
lazima uanze kwa mtaji mkubwa wa vifaa kamili vya mazoezi yaani (gym).
Hapana unaweza kuanza Kwa kuandaa sehemu tu na vyombo vya mziki ,pamoja
na mtu aliyevizuri katika swala zima la mazoezi.ukaongeza na ubunifu
wako kwani msingi mkubwa hapo ni ubunifu na ushawishi.
(9).KUANZISHA KAMPUNI YA KUCHORA MABANGO,KU design BLOGS, WEBSITES, LOGOS NA MICHORO YA MAJENGO
unachotakiwa
kufanya hapa nikuwatafuta watu wenye fani hizo na kuongea nao juu ya
hilo. Hutokosa watu wakufanya nao kwasababu kuna idadi kubwa ya watu
wasio na ajira..kisha unatakiwa uwe bize kuitangaza kampuni yako
mitandaoni ili ijulikane na watu wengi zaidi na kuongeza wateja..
(10).KUWA DALALI
Unachopaswa
kuwa nacho hapa ni uaminifu,lugha nzuri Kwa watu wote,umakini na
uchangamfu katika kusaka wateja.Mfano unaweza kuwa dalali kwa njia ya
uuzaji wa bidhaa kwa makubaliano ya mitandaoni, ukawa unalipwa kila
unapokamilisha dili.
(11).KUTOA USHAURI WA KITAALAMU
Kama
wewe ni mtu mwenye ujuzi maalumi juu ya jambo fulani, unaweza kuanzisha
sehemu maalum kwaajiri ya kutoa ushaur wa kitaalam juu ya swala
hilo...Mfano waliosoma maswala ya IT ni rahisi zaidi kupata wateja kwani
matumizi ya vifaa vya kiteknolojia yako juu sana siku hizi,na wengi wa
watumiaji hawana elimu yakutosha juu ya vifaa hivyo ,Kwa mantiki hiyo
hii nayo ni fursa..
(12).KUUZA UBUYU NA BIDHAA NYINGINE NDOGO NDOGO.
Kama
vile karanga na ice cream na biscuits.. Biashara hizi hulipa sana
.Mfano mfuko mmoja wa ubuyu unaweza kuununua Kwa tsh 1500/= mpaka 2000/=
na unaweza kufunga vipakti vya 6500 au 5500/= ukiangalia hapo bado
utaweza kuingiza faida itakayo kuwezesha kufikia malengo yako.
N.B:
kabla yakuanza jambo lolote kati ya hayo hakikisha una taarifa kamili
zifuatazo ;a) bidhaa husika zinapatikanaje? .b).soko lake likoje..c)wapi
kuliko na wahitaji zaidi...d).vitu gani au watu gani wa muhimu unapaswa
kuwa navyo kabla ya kuanzisha lolote...e).unaweza kuanzisha jambo Kwa
kuwaweka watu pamoja kwa maelewano ya malipo ya baada ya
kazi....f).utambue unataka nini ili iwe nini na kwa wakati
gani...g).mwisho kabisa iandae nafsi yako vizuri kukubaliana na lolote
litakalo jitokeza katika biashara yako..usiogope kukosea ila jifunze
zaidi.
Hongera kwa kukubali kujifunza elimu hii ndogo ya Ujasiriamali na utambuzi wa fursa........
IMEANDALIWA NA
Lufame TZ
Karibu tena kwa makala nzuri zaidi
No comments:
Post a Comment