BODI YA MIKOPO YAFUNGUA RASMI MFUMO WA UOMBAJI MIKOPO

BODI YA MIKOPO KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU NCHINI (HESLB)
Bodi hiyo inayohusika na kutoaji wa mikopo Kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini imetoa taarifa Kwa umma kuwa ,bodi hiyo itaanza kupokea maombi ya mikopo Kutoka Kwa wanafunzi watakao hitaji mikopo hiyo kwaajiri ya kusoma elimu ya juu.

Bodi hiyo imetangaza kuwa
wanafunzi wote wataanza kuomba mikopo kuanzia tarehe 06/08/2017 mpaka tarehe 04/09/2017

Miongoni mwa mambo ya msingi waliyo elekeza ni kwamba wanafunzi wanatakiwa kusoma Kwa umakini mwongozo wa uombaji mikopo k
Kwa mwaka mpya wa masomo (2017/2018)

Kusoma mwongozo na taarifa nyingine bofya link hiyo hapo nchini

https://olas.heslb.go.tz

Imetolewa na bodi ya mikopo Kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini (HESLB)

HATUA 10 MUHIMU ZA KUZINGATIA KABLA NA WAKATI WA KUOMBA MKOPO WA ELIMU YA JUU (2017/2018)

ZIFUATAZO NI HATUA 10 MUHIMU ZA KUZINGATIA

1. Soma Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa Mwaka 2017-18 kabla ya kufanya lolote.
2. Maombi yatapokelewa kwa njia ya mtandao kuanzia tarehe 6 Agosti – 4 Septemba,
2017;
3. Tembelea tovuti ya Bodi na kujisajili kwa kutumia Namba yako
ya Mtihani wa Kidato cha Nne;
4. Pata Namba ya Kumbukumbu ya Malipo/Reference Number (99117xxxxxxx) baada ya
kujisajili ambayo utaitumia kulipa TZS 30,000.00 kwa mkupuo mmoja kwa njia
zifuatazo:
• MPesa, AirtelMoney au TigoPesa kwa Namba ya Kampuni 888999. Baada ya
kulipa, utatumiwa stakabadhi yako kwa njia ya ‘sms’;
• Tumia Namba ya Kumbukumbu ya Malipo/Reference Number uliyopata kutoka
katika mtandao wa OLAMS kufanya malipo katika Tawi lolote au Wakala
yeyote wa Benki za CRDB na NMB. Ikiwa una swali, muulize Afisa wa
Benki.
5. Fungua mtandao wa OLAMS kwa ajili ya kuendelea na kujaza fomu ya maombi;
6. ‘Print’ fomu uliyokamilisha kujaza kwenye mtandao, ipeleke kwa Kamishna wa Viapo au
Wakili/Hakimu na Viongozi wa Serikali ya Mtaa wako kwa ajili ya saini;
7. Thibitisha nakala za vyeti vyote unavyoambatisha na fomu ya maombi kwa Kamishna wa
Viapo au Wakili/Hakimu;
8. ‘Upload’ kwenye mtandao (https://olas.heslb.go.tz) kurasa zote zilizosainiwa na
kugongwa mihuri pamoja na nakala zote za vyeti zilizothibitishwa na Kamishna wa Viapo
au Wakili/Hakimu;
9. Hakikisha unazo nyaraka zifuatazo/zitakazoambatanishwana ombi lako:
i. Fomu ya Maombi iliyosainiwa na Kamishna wa Viapo au Wakili/Hakimu;
ii. Nakala za vyeti vya taaluma zilizothibitishwa na kugongwa muhuri na
Kamishna wa Viapo au Wakili/Hakimu;
iii. Nakala ya cheti cha Kuzaliwa kilichothibitishwa na Wakala wa Usajili,
Ufilisi na Udhamini (RITA);
iv. Ikiwa ni yatima, nakala ya cheti/vyeti vya vifo vilivyothibitishwa na
Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA);
v. Ikiwa ulifadhiliwa, nakala ya barua kutoka taasisi iliyofadhili masomo; na
vi. Nyaraka nyingine muhimu zinazothibitisha uhitaji wako;
10. Toa nakala (photocopies) za nyaraka zote hapo juu kwa ajili ya kumbukumbu
yako. Fomu halisi ya maombi iliyosainiwa na Kamishna wa Viapo au Wakili/Hakimu
pamoja na nakala zilizothibitishwa (certified copies) zitumwe kwa njia ya EMS kwenda:
Mkurugenzi Mtendaji,
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu,
Kitalu Na. 8, Nyumba Na. 45,
Barabara ya Sam Nujoma, Mwenge,
S.L.P. 76068, DAR ES SALAAM.
Hakikisha bahasha inakuwa na fomu ya mwombaji mmoja, anuani ya muombaji
ikionyesha namba ya mtihani ya kidato cha nne na mwaka, pamoja na neno “maombi
ya mkopo”

Imetolewa na Bodi ya mikopo Kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini
(HELSB)

SIFA KUMI (10) ZA MSINGI ZA KUKUFANYA UPATE MKOPO WA ELIMU YA JUU (2017/2018)

JE, UTAOMBA MKOPO WA ELIMU YA JUU MWAKA HUU?
• ZIFUATAZO NI SIFA KUMI (10) ZA MSINGI
1. Mwombaji awe Mtanzania.
2. Mwombaji awe ameomba kudahiliwa na Chuo Kikuu au Taasisi ya Elimu
ya Juu inayotambuliwa na Serikali.
3. Asiwe mwanafunzi wa masomo ya jioni (Part time Student).
4. Asiwe na udhamini/ufadhili/msaada wa kifedha kutoka katika vyanzo
vingine.
5. Awe ameomba mkopo kupitia mfumo wa mtandao (OLAMS).
6. Awe amefaulu mitihani ya mwisho wa mwaka (wanaoendelea na masomo)
na matokeo yake kuwasilishwa Bodi ya Mikopo na chuo chake.
7. Awe amemaliza Kidato cha Sita au awe na sifa linganishi (kama Diploma
n.k) ndani ya miaka mitatu (2015/2016 – 2017/2018).
8. Awe na umri usiozidi miaka 30 wakati wa kufanya maombi.
9. Waombaji ambao wazazi wao ni Wakurugenzi au Mameneja Waandamizi
katika Makampuni binafsi yanayotambuliwa na Mamlaka za Mapato na
Usajili hawatarajiwi kuomba;
10.Waombaji ambao wazazi wao ni viongozi wa umma au kisiasa ambao
wanatajwa na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma hawatarajiwi
kuomba mikopo.
Mwisho wa kuomba mkopo in Septemba 4, 2017

Imetolewa na Bodi ya mikopo Kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini
HESLB