Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mitihani ya upimaji wa darasa la nne na kidato cha pili iliyofanyika Novemba 22 na 23 mwaka jana, matokeo hayo yameonesha kuwepo kwa ufaulu mkubwa.
Matokeo yametangazwa leo Jumatatu Januari 8,2018 na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema kuwa wanafunzi 1,086,156 waliofanya mtihani wa darasa la nne wamefaulu kati ya 1,158,444 waliofanya mtihani hiyo ya upimaji huo.
MATOKEO YA WANAFUNZI WA DARASA LA NNE WA 2017
MATOKEO YA KIDATO CHA PILI WA 2017
Aidha ameeleza kuwa wanafunzi walofaulu kwa kupata alama zenye madaraja ya A,B,C na D na wanafunzi 72,288 sawa na asilimilia 6.24 wamepata alama za daraja E, ambao ni ufaulu usioridhisha.
Kuhusu matokea ya upimaji wa kidato cha pili, Dk Msonde amesema jumla ya wanafunzi 433,453 sawa na asilimia 82.32 kati ya 486,742 waliosajiliwa kufanya mtihani huo wamepata ujuzi wa maarifa ya kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu.
Dk Msonde alisema wanafunzi wa kidato cha pili 51,807 sawa na asilimia 10.68 wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu.
Imetolewa na Baraza la mitihani Tanzania (NECTA)
NA KUANDIKWA NA
PETER LUGENDO .
ahsante kwa kutembelea blog hii, karibu tena kwa taarifa muhimu, Habari, na matukio mbali mbali. Ahsante
No comments:
Post a Comment