Tanzania na Kenya zinajitenga na Afrika? Ufa waibuka Bonde la Ufa na kuongeza uwezekano Afrika kugawanyika


Kuibuka kwa ufa mkubwa katika eneo la Suswa katika Bonde la Ufa kusini magharibi Emwa Kenya kumezua wasiwasi kuhusu uthabiti wa eneo la Afrika Mashariki kijiolojia.
Wataalamu wanasema kutokea kwa ufa huo katika jimbo la Nakuru ni shughuli ya kijiolojia inayochukua muda mrefu ambayo imekuwa ikiendelea kwa muda.
Hilo limezua hatari ya kuanza kutokea tena kwa mitetemeko ya ardhi na milipuko ya vilkano.
Wanajiolojia wanasema baada ya mamilioni ya miaka, bara la Afrika litapasuka na kuwa vipande viwili.
Mabaki ya binadamu 'wa kwanza' yapatikana Morocco
Kwa nini mji wa Jerusalem ni mtakatifu?
Kisiwa cha wanaume pekee chatambuliwa na Unesco
Shimo moto zaidi duniani lachimbwa Iceland
Sehemu ya mpasuko itakuwa kwenye Bonde la Ufa jambo ambalo linazua uwezekano wa Kenya na Tanzania, pamoja na mataifa mengine ya Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika, kujitenga na bara la Afrika.
Mwanajiolojia David Adede ameambia BBC kwamba ufa huo ni sehemu ya kutengana kwa vipande viwili vikubwa vya bara Afrika ambako kutasababisha bara Afrika kutengana na kuwa mabara mawili.
Amesema shughuli hiyo imekuwa ikiendelea kwa muda lakini dalili zake zilikuwa zinafichwa na majivu ya volkano ambayo polepole yamekuwa yakiziba ufa kila unapotokea.
"Maji ya mvua yamesomba majivu hayo pamoja na mchanga na kuufanya ufa huo kuonekana zaidi," amesema.
Haki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image caption
Ufa mkubwa umetokea kilomita 54 kusini magharibi mwa Nairobi katika Bonde la Ufa
Anasema vipande hivyo vimekuwa vikitengana "katika kasi ya sentimita mbili kila mwaka."
Kipande kilicho na sehemu kubwa ya bara hufahamika kama Kipande cha Nubia na kipande cha pili hufahamika kama Kipande cha Somalia.
Dkt James Hammond kutoka kwa Idara ya Sayansi na Uhandisi wa Dunia kutoka chuo cha Imperial College London alinukuliwa na jarida la mtandaoni la Mail & Guardian akisema: "Katika miaka milioni kadha ijayo, shughuli hii itakamilika na kuigawa Afrika mara mbili, na kuunda bahari mpya hapo katikati na bara jingine. Ukitumia jiografia ya sasa, bara hilo jipya litashirikisha Somalia, nusu ya Ethiopia, Kenya na Tanzania."
Makaburi yaliyo na 'ujumbe kutoka kuzimu' Misri
Kemikali inayounda sehemu ya ndani ya dunia
Baadhi ya wanajiolojia wanakadiria kwamba huenda mpasuko huu ukayabeba pia mataifa ya Uganda, Rwanda, Burundi na maeneo ya Malawi na Msumbiji.
Mwanajilojia Dereje Ayalew kutoka Chuo Kikuu cha Addis Ababa Ethiopia aliambia jarida hilo kwamba dalili za kutokea kwa bahari zimeanza kuonekana katika maeneo ya jangwani ya Ethiopia, eneo la Afar ambalo pia linahusisha baadhi ya maeneo ya Eritrea na Djibouti.

Mwaka 2005, alisema tayari nyufa nyingi zimeanza kutokea na ardhi imebonyea kwa hadi mira 100.
Ufa huo ulianza kuonekana wiki moja iliyopita baada ya mvua kubwa kunyesha na barabara ya Mai Mahiu kwenda Narok ikakatika eneo lenye ufa huo.
Awali, wengi waliamini ufa huo uliotokea Jumanne wiki iliyopita eneo la Karima ambalo linapatikana kilomita sita kutoka mji wa Mai Mahiu ulitokana na mvua kubwa.
Ufa huo uliokuwa umeikata barabara hiyo ulikuwa umeenea umbali wa mita 700.
Madini mapya yagunduliwa Tanzania
Maji ya kale zaidi yagunduliwa Canada
Maafisa wa Mamlaka ya Taifa ya Barabara Kenya (KeNHA) wakishirikiana na mkandarasi kutoka China anayejenga reli ya kisasa, walifika eneo hilo na kuziba ufa.
Baada ya uchunguzi, ilibainika kwamba ulitokana na shughuli ya kijiolojia chini ya ardhi ambayo ilihusisha mvutano wa vipande vikubwa vya ardhi.
Siku chache baadaye Jumapili, ufa huo uliendelea kupanuka na kuathiri barabara hiyo tena jambo lililosababisha magari yenye kubeba mizigo mizito kutoweza kupita.
Aidha, ufa huo ulianza kuathiri nyumba za wakazi.
"Mkandarasi na kundi la wahandisi wamewekwa hapo kwa sasa na watasalia kuendelea kufuatilia yanayojiri kutokana na shughuli za kivolkano ambazo zilisababisha ufa huo," alisema naibu mkurugenzi wa mawasiliano wa KeNHA Charles Njogu baada ya ukarabati huo mara ya kwanza.
Bw Adede amesema hatua ya kuziba ufa huo kwa sasa itasaidia kwa muda mfupi tu.
Ufa huo umepitia katika baadhi ya nyumba na mashamba ya watu.

Image caption
Bw Njoroge amelazimika kuhama kwake
Mmoja wa walioathirika ni Eliud Njoroge, 77, ambaye ameambia BBC kwamba ameishi eneo hilo kwa zaidi ya miaka 20.
Anasema amelazimika kuibomoa nyumba yake na sasa analazimika kuishi kama 'mkimbizi' kwa jirani yake.

Image caption
Ufa umegawa shamba hili lililopandwa maharagwe mara mbili
Mwandishi wa BBC aliyetembelea eneo hilo Gladys Njoroge anasema katika baadhi ya maeneo, ufa huo una upana wa mita 20 na kina cha hadi futi 50.

Image caption
Baadhi ya maeneo, ufa huo una kina cha zaidi ya futi 50
Wataalamu wametahadharisha kwamba nyufa zaidi zinaweza kuendelea kuonekana katika baadhi ya maeneo ya Bonde la Ufa.
Mwandishi wa BBC Ferdinand Omondi anasema viongozi wa eneo lililoathirika wamewahimiza wakazi wanaoishi karibu na maeneo yaliyotokea ufa huo kuhama, lakini baadhi kama Bw Njoroge hawawezi kuhamia mbali.

posted from Bloggeroid

WAZIRI DKT. MWAKYEMBE AMJIA JUU DIAMOND

Mwakyembe akerwa na Diamond, sasa kula naye sahani moja
Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameeleza kukerwa na mwanamuziki Diamond Platnumz kutokana na kumdharirisha Naibu wake, Juliana Shonza wakati akihojiwa katika kipindi cha The Play List cha Times FM na mitandaoni.

Katika maelezo yake Mwakyembe amesema kuwa inawezekana kwasasa Diamond ameanza kulewa sifa na umaarufu alionao mwanamuziki huyo.
Amesema kuwa serikali imekaa vikao vingi na wasanii lakini Diamond hahudhurii kwa hiyo si wajibu wa Serikali kumfanyia kikao chake mwenyewe kutokana na umaarufu wake.

“Hatuwezi kuwa na sheria kwa wasanii wengine na sheria maalum kwake, nadhani hizi ni dalili za kuanza kulewa umaarufu kwani Diamond si Kiongozi wa Shirikisho la Muziki wala msemaji wa Chama cha Muziki wa kizazi kipya kuwasemea wenzake,” amesema Dkt. Mwakyembe.

Hata hivyo, Dkt. Mwakuembe amemshauri mwanamuziki huyo asishindane na Serikali kama ana ushauri basi autoe kistaarabu ambao utazingatiwa lakini si kwa kumshambulia Naibu Waziri kwa dharau na kejeli jinsi alivyofanya, kitu ambacho amesema hajafurahishwa hata kidogo.

posted from Bloggeroid

TETESI ZA SOKA ULAYA

=Mshambulizi wa zamani wa Arsenal Thierry Henry anasema angependa kuchukua nafasi yake Arsene Wenger kama meneja wa Arsenal (Sky Sports).

= Chelsea ndio wako kifua mbele katika kumsaini mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski.
Mchezaji huyo raia wa Poland anataka kujiunga na Premier League. (Sun).

= AC Milan wana mpango wa kumsaini kiungo wa kati wa Swansea raia wa Korea Kusini Ki Sung-yueng, 29. (Calciomercato - in Italian) .

=Arsenal wanamtaka kiungo wa kati wa Paris St-Germain, Yacine Adli 27.

=Manchester City, Barcelona na Juventus pia wanamwinda raia huyo wa Ufaransa. (L'Equipe, via Sun).

= Washambuliaji wa Barcelona Lionel Messi, Luis Suarez na Philippe Coutinho wameidhinisha mipango ya klabu hiyo kuwaleta wachezaji watatu wapya msimu unaokuja. (Diario Gol - in Spanish) .

=Tottenham wanapanga kumsaini mshambulizi wa Sheffield United wa umri wa miaka 20 David Brooks. Klabu hiyo ya Premier League ina mpango wa kukubaliana pauni milioni 10 wa raia huyo wa Wales. (Sun).

= Kiungo wa kati wa Roma Radja Nainggolan alioneka kupoteza jino alipogongana na Franck Kessie wakati Roma ilishindwa na AC Milan siku ya Jumapili. (Football Italia).

= Mshambualiaji wa Paris St-Germain na Brazil Neymar, 26, amewaambia Real Madrid kuwa anataka pesa zaidi kuliko za mshambuliaji mreno Cristiano Ronaldo ili aweze kuhamia Bernabeu. (Sunday Express) .

=Kiungo wa kati mfaransa Paul Pogba yuko tayari kuondoka Manchester United ikiwa meneja Jose Mourinho ataendelea kuwepo Old Trafford. (Sun on Sunday) .

=Manchester United ni kati ya vilabu vikuu vinavyomtazana kiungo wa kati wa Lazio raia wa Serbia, Sergej Milinkovic-Savic, ambaye ambaye thamani yake huenda ikawa pauni mioni 80. (Sunday Mirror) .

=Meneja wa zamani wa Manchester United Louis van Gaal, huenda akachukua mahala pake Antonio Conte, huko Chelsea ikiwa uhusiao wake na Chlesea utazorota zaidi. (Sunday Mirror) Kwa hisani ya BBC.

posted from Bloggeroid

ASLAY, NANDY WATOZWA FAINI YA TSH MILLION 5

Wasanii wa muziki wa Bongo fleva nchini, Aslay na Nandy wamepigwa faini ya milioni 5 kwa kosa la kuimba wimbo wa Subalkheri bila kibali maalumu kutoka kwa watunzi na wamiliki wa wimbo huo ambao ni kikundi cha Utamaduni cha taarab asilia visiwani Zanzibar.

Kikundi hicho kilikusudia kuwafikisha mahakamani wasanii hao lakini kabla ya kuchukua hatu hiyo kiongozi wa Aslay na Nandy walifika visiwani humo na kufanya mazungumzo na kikundi hicho.

Ambapo viongozi hao walikiri kufanya kosa hilo la kukariri na kuimba wimbo huo bila kibali toka kwa wamiliki hao na kupitia kosa hilo kikundi hiko cha taarabu kimewataka walipwe milioni tano kama adhabu.

Katibu Mkuu wa kikundi cha utamaduni cha tarabu asilia, Taimur Rukuni Twaha, amesema kikundi hicho cha tarab kimewataka wasanii hao kulipa faini kutokana na kuimba wimbo huo bila ya ridhaaT.waha amesema licha ya kukiri makosa hayo pia meneja wa Aslay ameomba kuingia mkataba na kikundi hicho cha tarab kufanya biashara ya kuziimba tena nyimbo zao nyingine za zamani.

Katibu huyo amesema kuhusu nyimbo zao kuimbwa tena hilo bado hawajaafikiana kwa sababu walishapewa agizo na Rais mstaafu wa awamu ya tatu Dk Salmin Amour Juma wakati akiwa rais, kuwa wasikubali nyimbo zao za tarabu asilia kuzibadili na kuzifanya katika mfumo wa muziki wa kisasa.

posted from Bloggeroid

Magazeti ya Tanzania leo Januari 31, 2018



Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Januari 31 2018. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele.



posted from Bloggeroid

SHULE KUMI BORA NA SHULE KUMI ZA MWISHO KITAIFA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2017.

Katika matokeo hayo ya kidato cha nne, pamoja na kuwepo kwa upandaji wa ufaulu kwa asilimia 7, zipo shule zilizofanya vizuri zaidi kuliko nyingine na zile zilizofanya vibaya. Zifuatazo ni orodha ya shule 10, zilizofanya vizuri na zile zilizofanya vibaya.

Shule kumi (10) Bora kitaifa .

1. St. Francis Girls – Mbeya

2. Feza Boys – Dar es Salaam

3. Kemoboya – Kagera

4. Bethel Sabs Girls – Iringa

5. Anwarite Girls – Kilimanjaro

6. Marian Girls – Pwani

7. Canossa – Dar es salaam

8. Feza Girls – Dar es salaam

9. Marian Boys – Pwani

10. Shamsiye Boys – Dar es salaam


Shule Kumi (10) za Mwisho Kitaifa

1. Kusini – Kusini Unguja

2. Pwani Mchangani – Kaskazini Unguja

3. Mwenge SMZ – Mjini Magharibi

4. Langoni – Mjini Magharibi

5. Furaha – Dar es salaam

6. Mbesa – Ruvuma

7. Kabugaro – Kagera

8. Chokocho- Kusini Pemba

9. Nyeburu – Dar es salaam

10. Mtule – Kusini Unguja.
posted from Bloggeroid

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2017

Baraza la Mitihani Tanzania, limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na ule wa Maarifa (QT) leo juma nne 30,01,2018. Jijini Dar es salam .




Akitangaza matokeo hayo katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde ,amesema kuwa ufaulu wa wanafunzi kwa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 7 ukilinganisha na matokeo ya mwaka jana.

“Jumla ya Watahiniwa 287,713 ambao sawa na asilimia 77.09%  kwa shule za kawaida na vituo vya kujitegemea wamefaulu ambao katika ya hao wasichana wapo 143,728 sawa na asilimia 75.21% wakati wavulana wapo 143,985 sawa na asilimia 79.06%. Mwaka jana wanafunzi waliofaulu mitihani ya kidato cha nne walikuwa 277,283 ambao ni asilimia 70.09% hivyo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia"amesema MsondeBaraza la Mitihani Tanzania, limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na ule wa Maarifa (QT) leo juma nne 30,01,2018. Jijini Dar es salaam.
 
             KUYAONA MATOKEO HAYO BOFYA HAPA

.
Mbali na hilo Msonde aliweza kuweka wazi kuwa jumla ya wanafunzi 265 wamebainika kufanya udanganyifu mbalimbali katika mitihani hiyo ambayo ilianza kufanyika Oktoba 30, 2016 mpaka Novemba 17, 2016 .



Endelea kutembelea blog hii tuzidi kukujuza mengi yaliyojili, ndani na nje ya nchi.
By blogger Peter Lugendo
posted from Bloggeroid

MAKUBWA YAGUNDULIKA KUHUSU NABII TITO.

Baada ya Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma hapo jana,kumkamata Tito Onesmo,mtu aliyejitengenezea umaarufu na kujiita   "Nabii Tito",

kwa makosa kadhaa, ikiweno kuzidhalilisha dini nyingine kwa kutumia kitabu kitakatifu (Biblia) kwa kutoa tafsiri zisizo sahihi  na kujirekodi akifanya mambo yaliyo kinyume na maadili ya nchi.

 Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma, limepata taarifa ya uthibitisho kutoka kwa daktari kuhusu hali ya akili ya Tito Onesmo Machibya, anayejiita ‘nabii Tito’ kuwa ana ukichaa.

Akitoa taarifa mbele ya vyombo vya habari jana, Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Mroto amesema kuwa wamepokea taarifa kuwa mtu huyo amewahi kulazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mwaka 2014 kutokana na kuwa na ugonjwa wa akili. Alisema baada ya kuruhusiwa, ripoti ya daktari inaonesha kuwa alitakiwa kurejea hospitalini hapo lakini hakufanya hivyo.

Aidha, Kamanda Mroto ameeleza kuwa baada ya kumkamata Januari 16 mwaka huu, walimpeleka katika hospitali ya Milembe mjini hapo ambapo daktari alithibitisha kuwa ana ugonjwa wa akili.

“Katika uchunguzi wa awali, Tito Onesmo Machibya anaonekana kama ana historia ya ukichaa kwa mujibu wa taarifa za madaktari. Inaonekana tarehe June 23, 2014 aliwahi kufikishwa Muhimbili akamuona Daktari William,” alisema Kamanda Mroto.

“Tarehe 9 Julai, 2014 alitakiwa kurudi hospitalini hapo lakini mtu huyo hakuweza kurejea,” aliongeza.

Hata hivyo, Kamanda Mroto alieleza kuwa wanamshikilia mtu huyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi kufahamu watu anaofanya nao kazi. Pia, kutokana na usalama wake kwani mahubiri anayoyafanya mitaani yanayodhalilisha dini nyingine yanaweza kumsababishia hatari.

Mtu huyo amekuwa akitumia Biblia kutoa mahubiri ambayo yameelezwa kuwa ni yenye tafsiri ya upotoshaji, akisambaza vipeperushi pamoja na vipande vya video kwenye mitandao

MKURUGENZI MARA KUCHUNGUZWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Raphael Nyanda kutuma timu ya wakaguzi kwenda kufanya ukaguzi maalumu katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Butiama.

Amesema kuwa Halmashauri hiyo imekuwa na tabia ya kutumia fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo zinazotolewa na Serikali katika shughuli nyingine jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Butiama katika ukumbi wa chuo Kikuu cha Kilimo cha Mwalimu Nyerere.

Aidha, Majaliwa pia ameagiza kuchunguzwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Butiama, Solomon Ngiliule pamoja na Mweka Hazina wa Halmashauri, Masanja Sabuni na Ofisa Manunuzi wa Halmashauri  hiyo. Robert Makendo.

Hata hivyo ameongeza kuwa viongozi hao wanatakiwa wachunguzwe kutokana na matumizi yasiyoeleweka ya fedha za miradi ya maendeleo zinazotolewa na Serikali zikiwemo sh. milioni 12 walizotumia kuandaa profile ya Halmashauri hiyo

posted from Bloggeroid

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI NA DARASA LA NNE YATANGAZWA

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mitihani ya upimaji wa darasa la nne na kidato cha pili iliyofanyika Novemba 22 na 23 mwaka jana, matokeo hayo yameonesha kuwepo kwa ufaulu mkubwa.

Matokeo yametangazwa leo Jumatatu Januari 8,2018 na Katibu Mtendaji wa Necta,  Dk Charles Msonde amesema kuwa wanafunzi 1,086,156 waliofanya mtihani wa darasa la nne wamefaulu kati ya 1,158,444 waliofanya mtihani hiyo ya  upimaji huo.

MATOKEO YA WANAFUNZI WA DARASA LA NNE WA 2017

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI WA 2017

Aidha ameeleza kuwa  wanafunzi walofaulu kwa kupata alama zenye madaraja ya A,B,C na D na wanafunzi 72,288 sawa na asilimilia 6.24 wamepata alama za daraja E, ambao ni ufaulu usioridhisha.

Kuhusu matokea ya upimaji wa kidato cha pili, Dk Msonde  amesema jumla ya wanafunzi 433,453 sawa na asilimia 82.32 kati ya 486,742 waliosajiliwa  kufanya mtihani huo wamepata ujuzi wa maarifa ya kuwawezesha kuendelea  na kidato cha tatu.

Dk Msonde alisema wanafunzi wa kidato cha pili  51,807 sawa na asilimia 10.68 wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu.


Imetolewa na Baraza la mitihani Tanzania (NECTA)
NA KUANDIKWA NA
PETER LUGENDO .

ahsante kwa kutembelea blog hii, karibu tena kwa taarifa muhimu, Habari, na matukio mbali mbali. Ahsante