Magazeti ya Tanzania leo Januari 31, 2018



Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Januari 31 2018. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele.



posted from Bloggeroid

SHULE KUMI BORA NA SHULE KUMI ZA MWISHO KITAIFA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2017.

Katika matokeo hayo ya kidato cha nne, pamoja na kuwepo kwa upandaji wa ufaulu kwa asilimia 7, zipo shule zilizofanya vizuri zaidi kuliko nyingine na zile zilizofanya vibaya. Zifuatazo ni orodha ya shule 10, zilizofanya vizuri na zile zilizofanya vibaya.

Shule kumi (10) Bora kitaifa .

1. St. Francis Girls – Mbeya

2. Feza Boys – Dar es Salaam

3. Kemoboya – Kagera

4. Bethel Sabs Girls – Iringa

5. Anwarite Girls – Kilimanjaro

6. Marian Girls – Pwani

7. Canossa – Dar es salaam

8. Feza Girls – Dar es salaam

9. Marian Boys – Pwani

10. Shamsiye Boys – Dar es salaam


Shule Kumi (10) za Mwisho Kitaifa

1. Kusini – Kusini Unguja

2. Pwani Mchangani – Kaskazini Unguja

3. Mwenge SMZ – Mjini Magharibi

4. Langoni – Mjini Magharibi

5. Furaha – Dar es salaam

6. Mbesa – Ruvuma

7. Kabugaro – Kagera

8. Chokocho- Kusini Pemba

9. Nyeburu – Dar es salaam

10. Mtule – Kusini Unguja.
posted from Bloggeroid

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2017

Baraza la Mitihani Tanzania, limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na ule wa Maarifa (QT) leo juma nne 30,01,2018. Jijini Dar es salam .




Akitangaza matokeo hayo katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde ,amesema kuwa ufaulu wa wanafunzi kwa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 7 ukilinganisha na matokeo ya mwaka jana.

“Jumla ya Watahiniwa 287,713 ambao sawa na asilimia 77.09%  kwa shule za kawaida na vituo vya kujitegemea wamefaulu ambao katika ya hao wasichana wapo 143,728 sawa na asilimia 75.21% wakati wavulana wapo 143,985 sawa na asilimia 79.06%. Mwaka jana wanafunzi waliofaulu mitihani ya kidato cha nne walikuwa 277,283 ambao ni asilimia 70.09% hivyo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia"amesema MsondeBaraza la Mitihani Tanzania, limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na ule wa Maarifa (QT) leo juma nne 30,01,2018. Jijini Dar es salaam.
 
             KUYAONA MATOKEO HAYO BOFYA HAPA

.
Mbali na hilo Msonde aliweza kuweka wazi kuwa jumla ya wanafunzi 265 wamebainika kufanya udanganyifu mbalimbali katika mitihani hiyo ambayo ilianza kufanyika Oktoba 30, 2016 mpaka Novemba 17, 2016 .



Endelea kutembelea blog hii tuzidi kukujuza mengi yaliyojili, ndani na nje ya nchi.
By blogger Peter Lugendo
posted from Bloggeroid

MAKUBWA YAGUNDULIKA KUHUSU NABII TITO.

Baada ya Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma hapo jana,kumkamata Tito Onesmo,mtu aliyejitengenezea umaarufu na kujiita   "Nabii Tito",

kwa makosa kadhaa, ikiweno kuzidhalilisha dini nyingine kwa kutumia kitabu kitakatifu (Biblia) kwa kutoa tafsiri zisizo sahihi  na kujirekodi akifanya mambo yaliyo kinyume na maadili ya nchi.

 Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma, limepata taarifa ya uthibitisho kutoka kwa daktari kuhusu hali ya akili ya Tito Onesmo Machibya, anayejiita ‘nabii Tito’ kuwa ana ukichaa.

Akitoa taarifa mbele ya vyombo vya habari jana, Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Mroto amesema kuwa wamepokea taarifa kuwa mtu huyo amewahi kulazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mwaka 2014 kutokana na kuwa na ugonjwa wa akili. Alisema baada ya kuruhusiwa, ripoti ya daktari inaonesha kuwa alitakiwa kurejea hospitalini hapo lakini hakufanya hivyo.

Aidha, Kamanda Mroto ameeleza kuwa baada ya kumkamata Januari 16 mwaka huu, walimpeleka katika hospitali ya Milembe mjini hapo ambapo daktari alithibitisha kuwa ana ugonjwa wa akili.

“Katika uchunguzi wa awali, Tito Onesmo Machibya anaonekana kama ana historia ya ukichaa kwa mujibu wa taarifa za madaktari. Inaonekana tarehe June 23, 2014 aliwahi kufikishwa Muhimbili akamuona Daktari William,” alisema Kamanda Mroto.

“Tarehe 9 Julai, 2014 alitakiwa kurudi hospitalini hapo lakini mtu huyo hakuweza kurejea,” aliongeza.

Hata hivyo, Kamanda Mroto alieleza kuwa wanamshikilia mtu huyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi kufahamu watu anaofanya nao kazi. Pia, kutokana na usalama wake kwani mahubiri anayoyafanya mitaani yanayodhalilisha dini nyingine yanaweza kumsababishia hatari.

Mtu huyo amekuwa akitumia Biblia kutoa mahubiri ambayo yameelezwa kuwa ni yenye tafsiri ya upotoshaji, akisambaza vipeperushi pamoja na vipande vya video kwenye mitandao

MKURUGENZI MARA KUCHUNGUZWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Raphael Nyanda kutuma timu ya wakaguzi kwenda kufanya ukaguzi maalumu katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Butiama.

Amesema kuwa Halmashauri hiyo imekuwa na tabia ya kutumia fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo zinazotolewa na Serikali katika shughuli nyingine jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Butiama katika ukumbi wa chuo Kikuu cha Kilimo cha Mwalimu Nyerere.

Aidha, Majaliwa pia ameagiza kuchunguzwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Butiama, Solomon Ngiliule pamoja na Mweka Hazina wa Halmashauri, Masanja Sabuni na Ofisa Manunuzi wa Halmashauri  hiyo. Robert Makendo.

Hata hivyo ameongeza kuwa viongozi hao wanatakiwa wachunguzwe kutokana na matumizi yasiyoeleweka ya fedha za miradi ya maendeleo zinazotolewa na Serikali zikiwemo sh. milioni 12 walizotumia kuandaa profile ya Halmashauri hiyo

posted from Bloggeroid

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI NA DARASA LA NNE YATANGAZWA

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mitihani ya upimaji wa darasa la nne na kidato cha pili iliyofanyika Novemba 22 na 23 mwaka jana, matokeo hayo yameonesha kuwepo kwa ufaulu mkubwa.

Matokeo yametangazwa leo Jumatatu Januari 8,2018 na Katibu Mtendaji wa Necta,  Dk Charles Msonde amesema kuwa wanafunzi 1,086,156 waliofanya mtihani wa darasa la nne wamefaulu kati ya 1,158,444 waliofanya mtihani hiyo ya  upimaji huo.

MATOKEO YA WANAFUNZI WA DARASA LA NNE WA 2017

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI WA 2017

Aidha ameeleza kuwa  wanafunzi walofaulu kwa kupata alama zenye madaraja ya A,B,C na D na wanafunzi 72,288 sawa na asilimilia 6.24 wamepata alama za daraja E, ambao ni ufaulu usioridhisha.

Kuhusu matokea ya upimaji wa kidato cha pili, Dk Msonde  amesema jumla ya wanafunzi 433,453 sawa na asilimia 82.32 kati ya 486,742 waliosajiliwa  kufanya mtihani huo wamepata ujuzi wa maarifa ya kuwawezesha kuendelea  na kidato cha tatu.

Dk Msonde alisema wanafunzi wa kidato cha pili  51,807 sawa na asilimia 10.68 wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu.


Imetolewa na Baraza la mitihani Tanzania (NECTA)
NA KUANDIKWA NA
PETER LUGENDO .

ahsante kwa kutembelea blog hii, karibu tena kwa taarifa muhimu, Habari, na matukio mbali mbali. Ahsante