BODI YA MIKOPO YAFUNGUA RASMI MFUMO WA UOMBAJI MIKOPO

BODI YA MIKOPO KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU NCHINI (HESLB)
Bodi hiyo inayohusika na kutoaji wa mikopo Kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini imetoa taarifa Kwa umma kuwa ,bodi hiyo itaanza kupokea maombi ya mikopo Kutoka Kwa wanafunzi watakao hitaji mikopo hiyo kwaajiri ya kusoma elimu ya juu.

Bodi hiyo imetangaza kuwa
wanafunzi wote wataanza kuomba mikopo kuanzia tarehe 06/08/2017 mpaka tarehe 04/09/2017

Miongoni mwa mambo ya msingi waliyo elekeza ni kwamba wanafunzi wanatakiwa kusoma Kwa umakini mwongozo wa uombaji mikopo k
Kwa mwaka mpya wa masomo (2017/2018)

Kusoma mwongozo na taarifa nyingine bofya link hiyo hapo nchini

https://olas.heslb.go.tz

Imetolewa na bodi ya mikopo Kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini (HESLB)

HATUA 10 MUHIMU ZA KUZINGATIA KABLA NA WAKATI WA KUOMBA MKOPO WA ELIMU YA JUU (2017/2018)

ZIFUATAZO NI HATUA 10 MUHIMU ZA KUZINGATIA

1. Soma Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa Mwaka 2017-18 kabla ya kufanya lolote.
2. Maombi yatapokelewa kwa njia ya mtandao kuanzia tarehe 6 Agosti – 4 Septemba,
2017;
3. Tembelea tovuti ya Bodi na kujisajili kwa kutumia Namba yako
ya Mtihani wa Kidato cha Nne;
4. Pata Namba ya Kumbukumbu ya Malipo/Reference Number (99117xxxxxxx) baada ya
kujisajili ambayo utaitumia kulipa TZS 30,000.00 kwa mkupuo mmoja kwa njia
zifuatazo:
• MPesa, AirtelMoney au TigoPesa kwa Namba ya Kampuni 888999. Baada ya
kulipa, utatumiwa stakabadhi yako kwa njia ya ‘sms’;
• Tumia Namba ya Kumbukumbu ya Malipo/Reference Number uliyopata kutoka
katika mtandao wa OLAMS kufanya malipo katika Tawi lolote au Wakala
yeyote wa Benki za CRDB na NMB. Ikiwa una swali, muulize Afisa wa
Benki.
5. Fungua mtandao wa OLAMS kwa ajili ya kuendelea na kujaza fomu ya maombi;
6. ‘Print’ fomu uliyokamilisha kujaza kwenye mtandao, ipeleke kwa Kamishna wa Viapo au
Wakili/Hakimu na Viongozi wa Serikali ya Mtaa wako kwa ajili ya saini;
7. Thibitisha nakala za vyeti vyote unavyoambatisha na fomu ya maombi kwa Kamishna wa
Viapo au Wakili/Hakimu;
8. ‘Upload’ kwenye mtandao (https://olas.heslb.go.tz) kurasa zote zilizosainiwa na
kugongwa mihuri pamoja na nakala zote za vyeti zilizothibitishwa na Kamishna wa Viapo
au Wakili/Hakimu;
9. Hakikisha unazo nyaraka zifuatazo/zitakazoambatanishwana ombi lako:
i. Fomu ya Maombi iliyosainiwa na Kamishna wa Viapo au Wakili/Hakimu;
ii. Nakala za vyeti vya taaluma zilizothibitishwa na kugongwa muhuri na
Kamishna wa Viapo au Wakili/Hakimu;
iii. Nakala ya cheti cha Kuzaliwa kilichothibitishwa na Wakala wa Usajili,
Ufilisi na Udhamini (RITA);
iv. Ikiwa ni yatima, nakala ya cheti/vyeti vya vifo vilivyothibitishwa na
Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA);
v. Ikiwa ulifadhiliwa, nakala ya barua kutoka taasisi iliyofadhili masomo; na
vi. Nyaraka nyingine muhimu zinazothibitisha uhitaji wako;
10. Toa nakala (photocopies) za nyaraka zote hapo juu kwa ajili ya kumbukumbu
yako. Fomu halisi ya maombi iliyosainiwa na Kamishna wa Viapo au Wakili/Hakimu
pamoja na nakala zilizothibitishwa (certified copies) zitumwe kwa njia ya EMS kwenda:
Mkurugenzi Mtendaji,
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu,
Kitalu Na. 8, Nyumba Na. 45,
Barabara ya Sam Nujoma, Mwenge,
S.L.P. 76068, DAR ES SALAAM.
Hakikisha bahasha inakuwa na fomu ya mwombaji mmoja, anuani ya muombaji
ikionyesha namba ya mtihani ya kidato cha nne na mwaka, pamoja na neno “maombi
ya mkopo”

Imetolewa na Bodi ya mikopo Kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini
(HELSB)

SIFA KUMI (10) ZA MSINGI ZA KUKUFANYA UPATE MKOPO WA ELIMU YA JUU (2017/2018)

JE, UTAOMBA MKOPO WA ELIMU YA JUU MWAKA HUU?
• ZIFUATAZO NI SIFA KUMI (10) ZA MSINGI
1. Mwombaji awe Mtanzania.
2. Mwombaji awe ameomba kudahiliwa na Chuo Kikuu au Taasisi ya Elimu
ya Juu inayotambuliwa na Serikali.
3. Asiwe mwanafunzi wa masomo ya jioni (Part time Student).
4. Asiwe na udhamini/ufadhili/msaada wa kifedha kutoka katika vyanzo
vingine.
5. Awe ameomba mkopo kupitia mfumo wa mtandao (OLAMS).
6. Awe amefaulu mitihani ya mwisho wa mwaka (wanaoendelea na masomo)
na matokeo yake kuwasilishwa Bodi ya Mikopo na chuo chake.
7. Awe amemaliza Kidato cha Sita au awe na sifa linganishi (kama Diploma
n.k) ndani ya miaka mitatu (2015/2016 – 2017/2018).
8. Awe na umri usiozidi miaka 30 wakati wa kufanya maombi.
9. Waombaji ambao wazazi wao ni Wakurugenzi au Mameneja Waandamizi
katika Makampuni binafsi yanayotambuliwa na Mamlaka za Mapato na
Usajili hawatarajiwi kuomba;
10.Waombaji ambao wazazi wao ni viongozi wa umma au kisiasa ambao
wanatajwa na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma hawatarajiwi
kuomba mikopo.
Mwisho wa kuomba mkopo in Septemba 4, 2017

Imetolewa na Bodi ya mikopo Kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini
HESLB

BREAKING NEWS: BEI ZA APPLICATION ZA CHUO ZA SHUKA RASMI.

Hii ni baada ya gharama za kuomba nafasi za chuo kuonekana zikiwa juu,na kulalmikiwa na wadau mbali mbali wa elimu na wananchi ,sasa serikali kupitia mamlaka inayohusika na vyuo vikuu nchini TCU ,imeamua kuingilia kati swala hilo na kutoa bei elekezi kwa vyuo vyote nchini,kuwa application form za vyuo vyote zitolewe kwa Tsh 10,000/= tu.
Kutoka Tsh 30,000/= iliyokuwa ikitozwa na vyuo vingi nchini.

Wanafunzi wote kuanzia Jana walianza kufaidika na punguzo hilo la bei za kupata form za kuomba nafasi za vyuo nchini .kwa Tsh 10,000/=

Imetangazwa rasmi na TCU .

Ahsante sana kwa kutembelea blog yangu .endelea kutembelea blog hii Mara kwa Mara uwe wakwanza kupata taarifa mbali mbali muhimu. Huruhusiwi kukopi au kupest taarifa yoyote kwenye blog hii bila idhini ya blogger
Peter Lugendo.
www.lufametz@gmailcom
www.facebook.com/lufametz
www.YouTube.com/lufameTV

TAARIFA MUHIMU KWA UMMA:VYUO NA PROGRAMU ZILIZOZUILIWA KUDAHILI WANAFUNZI WA MWAKA WA MASOMO 2017/2018


TAARIFA KWA UMMA
VYUO NA PROGRAMU ZILIVYOZUILIWA KUDAHILI
WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA KWA MWAKA
WA MASOMO 2017/18

PROGRAMU ZILIZOFUNGIWA NA MAJINA YA VYUO HUSIKA HAYA HAPA

Programu Jina la Chuo 

1. Master of Medicine Obstetrics and Gynecology -Hubert Kairuki Memorial University 

2. Master of Medicine General Surgery-Hubert Kairuki Memorial University 

3. Master of Medicine Internal Medicine -Hubert Kairuki Memorial University 

4. Master of Medicine Pediatric and child Health -Hubert Kairuki Memorial University 

5. Master of social Work -Hubert Kairuki Memorial University 

6. Master of Science in Public Health -Hubert Kairuki Memorial University 

7. Bachelor of Arts in Sociology -Jordan University College 

8. Bachelor of Arts in Philosophy- Jordan University College 

9. Bachelor of Arts in African Studies -Jordan University College 

10. Bachelor of Business Administration -Jordan University College 

11. Bachelor of Arts in Economics -Jordan University College 

12. Bachelor of Science in Psychology and Counselling-Jordan University College 

13. Bachelor of Accounting and Finance -Jordan University College 

14. Bachelor of Commerce and Accounts -St. Joseph University College of Management and 
Commerce 

15. Bachelor of Business Administration -St. Joseph University College of Management and 
Commerce 

16. Bachelor of Laws-Tumaini University Makumira 

17. Bachelor of Arts Music-Tumaini University Makumira 

18. Bachelor of Arts Languages -Tumaini University Makumira 

19. Bachelor of Science in Computer and Information Management- Tumaini University Makumira

20. Bachelor of Business Administration (Accounting) -Tumaini University Makumira 

21. Bachelor of Christian Education- Mount Meru University 

22. Bachelor of Arts in Human Resource Management-Mount Meru University 

23. Bachelor of Arts in Community Development -Mount Meru University 

24. Bachelor of Science with Education-Mount Meru University 

25. Bachelor of Education in Information Communication Technology -Mount Meru University 

26. Bachelor of Theology-Mount Meru University 

27. Master of Bussiness Administration(Cooperate Management) Mzumbe University - Mbeya University College 

28. Bachelor of Business Administration-Mount Meru University(Mwanza Centre) 

29. Bachelor of Arts With Education- Mount Meru University (Mwanza Centre) 

30. Bachelor of Education -Mount Meru University (Mwanza Centre) 

31. Bachelor of Business Administration (Accounting and Finance) -Mount Meru University -(Arusha Town Centre) 

32. Bachelor of Business
Administration (Marketing) -( Mount Meru University (Arusha Town Centre)

33. Bachelor of Arts in Philosophy with Ethics -Mwenge Catholic University

34. Bachelor of Environmental Health Sciences with Information 
Technology -
Ruaha Catholic University 

35. Bachelor of Business Administration -St. Johns University of Tanzania 

36. Bachelor of Accounting and Finance- St. Johns University of Tanzania 

37. Bachelor of Commerce with Education-St. Johns University of Tanzania 

38. Bachelor of Arts in Theology -St. Johns University of Tanzania

39. Master of Art theology and contemporary issues -St. Johns University of Tanzania 

40. Master of Business Administration-St. Johns University of Tanzania 

41. Master of Community development -St. Johns University of Tanzania 

42. Master of Science in Accounting- St. Johns University of Tanzania 

43. Master of Science in Finance-St. Johns University of Tanzania 

44. Master of Art in Education -St. Johns University of Tanzania 

45. Bachelor of Science in Mental Health and Rehabilitation -Sebastian Kolowa Memorial University 

46. Bachelor of Arts in Mass Communication-Stefano Moshi Memorial University College 

47. Master of Business Administration -Tumaini University Dar es Salaam College 

48. Bachelor of Arts Sociology and Social Work-Teofilo Kisanji University Dar es Salaam College 

49. Bachelor of Education-University of Arusha (Buhare Centre) 

50. Bachelor of Science in Information Technology-University of Iringa 

51. Bachelor of Science in Computer Science Abdulrahman -Al- Sumait Memorial University (SUMAIT) 

52. Bachelor of Science in Information Technology Abdulrahman-Al- Sumait Memorial University (SUMAIT) 

53. Bachelor of Science with Education-Muslim University of Morogoro (MUM) 

54. Bachelor of Languages and Interpretation -Muslim University of Morogoro (MUM) 

55. Bachelor of Arts in Mass Communication -Muslim University of Morogoro (MUM) 

56. Bachelor of Islamic Studies with Education-Muslim University of Morogoro (MUM) 

57. Bachelor of Business Studies- Muslim University of Morogoro (MUM)

58. Bachelor of Science in Agricultural Engineering and Mechanization- University of Dar es Salaam 

59. Doctor of Medicine- University of Dar es Salaam 

60. Bachelor of Science in Petroleum Engineering -University of Dodoma 

61. BCOM in Management Science (Information Systems Management)- University of Dodoma 

62. Bachelor of Arts in Office Management and Administration- Stefano Moshi Memorial University College 

63. Bachelor of Business Administration- St. Johns University of Tanzania 

64. Postgraduate Diploma in Education-Ruaha Catholic University 

65. Master of Arts in Education- Ruaha Catholic University 

66. Master of Arts in Journalism and media Management-University of Iringa 

67. Master of Arts in Linguistics- Ruaha Catholic University 

68. Postgraduate Diploma in Law- Ruaha Catholic University 

69. Master of Law- Ruaha Catholic University 

70. PhD in Law -Ruaha Catholic University 

71. Master of Arts in Philosophy- Jordan University College 

72. Master of Arts in Sociology -Jordan University College 

73. Master of Education -Jordan University College 

74. Master of Arts in Tourism, Culture and Society-University of iringa

75. Bachelor of Science in Nursing Education- Institute of Social Welfare 

Imetolewa na: 
Prof. Eleuther Mwageni 
Kaimu Katibu Mtendaji 
24 Julai 2017.

Ahsante kwa kutembelea blog yangu .Endelea kutembelea Mara Kwa Mara uwe wa kwanza kupata habari na taarifa zote muhimu

Imeandikwa na blogger
Peter Lugendo 
CHANZO CHA HABARI NI TCU 
www.tcu.go.tz
Tutembelee kupitia 
www.facebook.com/lufametz
www.lufametz@gmail.com
www.YouTube.com/lufame TV

MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUWA NAYO WAKATI WA KU-APPLY CHUO NA GHARAMA ZAKE

Uhali gani mpenzi msomaji wa blog yangu,natumai umzima wa afya tele karibu katika muendelezo wa taarifa muhimu zinazoendelea kutolewa na blog yangu.
Kwanza kabisa ,napenda kuwapongeza wote mliofanikiwa kutimiza vigezo vinavyo hitajika kudahiliwa na vyuo mbali mbali nchini,kwaajiri ya kujiunga na elimu ya vyuo vikuu nchini,kwa mwaka mpya wa masomo 2017/2018.

  Leo blog yako ya Lufametz ,katika muendelezo wake wa kukupa taarifa muhimu ,tunakuletea taarifa muhimu Kwa mtu yeyote anayetaka ku-apply chuo chochote nchini.

A. MAHITAJI MUHIMU WAKATI WA KU-APPLY
      1).Passport size
           Katika kila chuo utakacho omba utatakiwa kuambatanisha na picha yako passport size  (1),muombaji au mtu anayekusaidia kufanya maombi atatakiwa kui-scan picha hiyo na kuiambatanisha kwenye form yako ya maombi.
      2).Namba zako za mtihani wa kidato cha nne na cha sita
        NB: Kwa wale watakao omba degree Kwa kutumia  cheti cha diploma watatakiwa kuomba kwanza NACTE (gharama ni 20,000/=) ili apewe code number yake ,ambayo ndiyo atakayo itumia kuomba degree.
   Pia kwa wale walio rudia mtihani watatakiwa kuandika namba zao za mitihani yote ya kwanza na ile aliyorudia.
     3).Taarifa zako binafsi
          -Tarehe yako ya kuzaliwa
          -mwezi na mwaka
       4). Email na namba yako ya Simu
              Hii pia huitajika wakati wa kuomba. Kwani hutumika baadae kwaajiri ya kukupa taarifa muhimu za chuo.
        5) Pesa
               Unashauriwa kuandaa pesa kuanzia Tsh 150,000/= Kwa wale watakao taka kuomba kwenye vyuo votano . Pesa hizo ni lazima ziwe kwenye account itakayo tumika kulipia form hiyo. Kwa mantiki hiyo unashauriwa pesa hizo ziwe kwenye account ya Tigo pesa, M.pesa airtel money n.k

B.GHARAMA ZA FORM HIZO ZA KUOMBA NAFASI ZA CHUO
      Baada ya kwa mabadiliko haya yaliyoko sasa .kila muombaji atatakiwa kuomba kwenye chuo husika moja Kwa moja ,na malipo yatafanyika kwenye chuo hicho kulingana na bei walizojiwekea .

 Ila mpaka sasa 90% ya vyuo vyote nchini, vinatoa form hizo Kwa Tsh 30,000/= mfano .UDOM 30,000/=
             MZUMBE  30,000/=
             UNIVERSITY OF IRINGA 30,000/=  N.K

C.IDADI YA FACULTY (KOZI ) UNAZO RUHUSIWA KUOMBA KWENYE CHUO KIMOJA
        90% Ya vyuo vyote nchini vinatoa nafasi tano. Kwahiyo muombaji ataweza kuomba faculty tano tofauti kwenye chuo kimoja.

D.MUDA ULIYOTOLEWA  KU-APPLY
         kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyo tangazwa na TUC .vyuo vitaendelea kupokea maombi kuanzia tar 22/07/2017 mpaka tar 30/08/2018 .ikiwa ni zaidi ya mwezi mmoja.


USHAURI
 Kabla ya ku-apply chuo chochote nchini. Hakikisha umepitia vizuri kitabu cha maelekezo kilichotolewa na TUC (TCU guide book) ukizingatia mambo muhimu yafuatayo;
  a).Je kwenye faculty unayotaka kuomba umetimiza vigezo vinavyo hitajika kwa ufasaha?
  b).Je faculty unayotaka kuomba inatolewa kwenye chuo hicho?
  c).Je unataarifa muhimu juu ya faculty unayoitaka?

Kama moja kati ya hayo bado hauko vizuri ni bora utulie kwanza ufanye uhakiki wa taarifa zako kabla hujajaza kuomba nafasi. Kwani unaweza kupoteza pesa bila mafanikio yoyote. Usikurupuke kuchukua maamuzi haraka bila kujiridhisha kwani hapo unachagua maisha yako ya baadae. Muda bado upo wa kutosha ni zaidi ya mwezi tulia ufanye chaguzi sahihi sehemu sahihi.

Ahsante sana Kwa kutembelea blog yangu. Natumai umefanikiwa na kufaidika kupitia chapisho hili .karibu tena Kwa taarifa muhimu zinazotolewa na blog yangu hii.

Huruhusiwi kukopi wala kupest taarifa yoyote kwenye blog hii, bila idhini ya mmiliki wa blog hii **Peter Lugendo ***
www.lufametz@gmail.com
www.Facebook.com/lufametz
www.YouTube.com/lufame TV

REYVANNY AWEKA HISTORIA MPYA KWENYE MUZIKI WA TANZANIA



Msanii anayepanda Kwa kasi kwenye industry ya muziki wa bongo fleva nchini ,Kutoka WCB

Reryvany ,ameweka historia mpya kwenye ramani ya muziki wa Tanzania baada ya kunyakuwa TUZO za BET yaani
(BLACKS ENTERTAINMENT TELEVISION). kwenye kategoria ya '" VIEWER'S CHOICE INTERNATIONAL ACT ARTIST''". Akiwashinda wasanii maarufu afrika kama Tekno wa Nigeria na stone boy.REYVANNY amekuwa msanii wa Kwanza Mtanzania kunyakuwa TUZO kwenye kinyang'anyiro hicho toka kuanzishwa Kwa tuzo hizo..


TAZAMA ALICHOKISEMA DIAMOND PLATNUMZ BAADA YA REYVANNY KUNYAKUWA TUZO HIYO.

Hiki ndicho alicho kiandika diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram

Mmmmh kaka diamond wewe Mungu anakuona ,ulimlenga nani kwani au ndiyo furaha mpaka imepitiliza!!

Hongera sana kaka diamond Kwa kumshika mkono kijana mwenzetu ila hongera nyingi zimuendee REYVANNY Kwa kujituma na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania..

posted from Bloggeroid
posted from Bloggeroid

SOMA HAPA VICHWA VYA HABARI VILIVYO TAWALA MAGAZETI YA LEO JUNE 24

Yamkini kutokana na sababu mbali mbali za kimaisha ,hukuweza kupitia magazetini na kujua yaliyoandikwa Leo hii...ila hujachelewa bado lufame tz tumekusogezea karibu yako ..


Bofya Link hiyo hapo usome yote yaliyomo magazetini Leo

Í


http://millardayo.com/mgnewjune24/

posted

posted from Bloggeroid

SOMA MAGAZETI YA LEO JUNE 24 HAPA

SHABIKI MAARUFU WA KLABU YA YANGA FC AIAGA DUNIA KWA AJARI YA GARI

Mshabiki maarufu nchini wa timu ya Yanga ALLY YANGA, amepoteza maisha Leo hii 20/06/2017 , kwa ajari ya gari huko mkoani Dodoma maeneo ya ipogoro alipokuwa kwenye mbio za mwenge.





Kwa watu wote ambao ni wanafamilia wa michezo nchini ,basi jina la
ALLY YANGA halitakuwa geni masikioni mwake ,ni mshabiki aliyejizolea umaarufu mkubwa kwenye soka la Tanzania hasa kutokana na tabia yake ya kuifuata timu hiyo popote inapo enda huku akiwa amejipaka rangi mwilini mwake.
.

MUNGU AILAZE PEMA PEPONI ROHO YA ALLY YANGA-- AMEN
posted from Bloggeroid

MAJINA YA WANAFUNZI WALIO CHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018

Majina ya wanafunzi waliopangiwa shule Kujiunga na kidato cha tano 2917/2018 yametolewa rasmi Leo ...
Nasi tumekuletea update kamili Kutoka TAMISEMI...

KUYAONA MAJINA HAYO
BONYEZA LINK HIYO HAPO CHINI

http://www.tamisemi.go.tz/form_five_selection_or/

HONGERA KWA KUTEMBELEA BLOG YANGU....Endelea KUTEMBELEA zaidi ujue mengi zaidi....www.lufametz.blogspot.com

posted from Bloggeroid

ni channel mpya kabisa imekufikia mbaka pale ulipo kaa mkao wakula kwa taarifa na burudani tembelea www.lufame.blogspot.co

 
HII NDIO MANDHARI YA MJI WA KAHAMA KARIBU SANA KWA BIASHARA